Boseman alipata umaarufu kote duniani baada yakuigiza katika filamu yakihistoria ya Black Panther, ambayo kinyume ya matarajio, filamu hiyo ilivunja rekodi nyingi za mauzo ya tiketi za watu walio itazama.
Waigizaji wenza wa filamu hiyo pamoja na mashabiki wao, wame endelea kutuma risala zao wiki moja baada ya kifo cha mpendwa wao. Wengi wao wame changia hisia zao na jinsi Boseman alivyo kuwa na maana kubwa katika maisha yao.
Katika taarifa iliyo chapishwa kwenye mitandao yakijamii, imebainika kuwa Boseman alikuwa akikabiliana na saratani kali wakati alikuwa akishiriki katika filamu ya Black Panther na zingine alizo igiza ndani. Vita vyake dhidi ya saratani hiyo vili isha 28 Agosti 2020, akiwa na umri wa miaka 44.