Katika mechi ya kwanza ya kombe la dunia la FIFA ya wanawake, wenyeji New Zealand walishinda mechi yao dhidi ya Norway kwa goli moja kwa sufuri.
Muda mfupi baadae wenyeji wenza wa kombe hilo Australia, waliwakaribisha Ireland dimbani mjini Sydney na katika dakika ya 52 uwanja huo na taifa lili lipuka kwa sherehe baada ya Stephanie Catley kufunga goli la kwanza na lapekee katika mechi hiyo kupitia mkwaju wa penati.
Katika kundi mechi ya pili ya kundi B Nigeria na Canada walimaliza mechi hiyo kwa sare ya kutofungana licha ya timu zote kuwa na fursa nyingi zakufunga goli.
Tuta kuletea matokeo ya mechi zingine punde tutakapo yapata.