Wapiga kura wamwadhibu Theresa May

Wachambuzi wengi wamaswala yakisiasa walisema ni uchaguzi ambao hau hitajiki, wakati mgombea wa chama cha Labour cha Uingereza Jeremy Corbyn alisema "ni uchaguzi ulio itishwa kwa ajili yakuongeza madaraka ya waziri mkuu Theresa May."

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ashindwa kupata viti vingi bungeni katika uchaguzi mkuu kama alivyo tarajia. Source: Picha:AAP

Kabla ya uchaguzi mkuu waziri mkuu alikuwa akiongoza katika kura ya maoni kwa 16% dhidi ya kiongzi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn. Wachambuzi wengi wa maswala yaki siasa na baadhi ya mashirika ya habari yalikuwa yana dai Bw Corbyn hawezi fanikiwa katika uchaguzi mkuu.

Ila baada ya wiki kadhaa za kampeni nchini kote, wapiga kura na wachambuzi walisubiri kuona iwapo utabiri wao utatimia.

Jeremy Corbyn and Theresa May
British Prime Minister Theresa May, right, is facing pressure to resign after her election gamble fails. Source: AAP

Kura zamaoni zilizo chapishwa siku na masaa kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu, zilikuwa zime zua wasi wasi miongoni mwa wanachama wa Conservatives na Waziri Mkuu, kwa sababu ya kasi ya ongezeko la umaarufu wa kiongozi wa upinzani.

Wagombea wawili wakubwa walisalia na matumaini yaku unda serikali punde baada ya kura kuhesabiwa.

Kura zilipo anza kuhesabiwa, chama cha Labour kilifanikiwa kushinda viti vya ubunge ambavyo chama tawala cha Conservatives kilikuwa kiki lenga, na hata baadhi ya wabunge wa Conservative walipoteza viti vyao vya ubunge dhidi ya wagombea wa Labour. Matarajia ya chama cha Conservative kuunda serikali ya wengi ilimwagiwa maji baridi punde baadae, na badala yake mazungumzo ya uwezekano waku unda serikali ya wachache kwa msaada wa vyama vidogo yali tarajiwa kuanza kwa kina.

Kabla ya jua kuchomoja, ilitangazwa hakuna chama kilicho fanikiwa kupata kura zakutosha kuunda serikali bila msaada, na punde baadae uvumi kuhusu uwezekano wa Waziri Mkuu Theresa May kujiuzulu ulianza kusambaa.

Waziri Mkuu Theresa May na mume wake Philip punde baada yaku piga kura.
Waziri Mkuu Theresa May na mume wake Philip punde baada yaku piga kura, katika uchaguzi mkuu katika kijiji cha Sonning Uingereza. Source: Press Association

Wakati huo huo kiongozi wa chama cha Labour, Jeremy Corbyn pamoja na wanachama wenza, wana endelea kusherekea matokeo ambayo chama hicho kime pata, ambayo ni mazuri kuliko ilivyo kuwa imetabiriwa.

Image

Baadhi ya wanachama wa Labour na wachambuzi wa maswala yaki siasa, wanatarajia Bw Corbyn ata unda serikali iwapo Theresa May, ata feli kupata idadi ya wabunge anao hitaji kuunda serikali.

 


Share

1 min read

Published

Updated

By SBS Swahili

Presented by SBS Swahili

Source: SBS Swahili




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service