Kijana toka timu ya Paris Saint-Germain, Mbappe, amekuwa nyota katika michuano hiyo ya Urusi, akifunga mara tatu, ukijumuisha umahiri aliouonyesha dhidi ya Argentina kwenye mzunguko wa 16.
Kocha mkuu Didier Deschamps aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano kabla ya mazoezi hayo kuwa, anatarajia kuwa na kikosi chake kamili kukabiliana na vijana wa Roberto Martinez na akafafanua kuwa, wachezaji wamepumzishwa mazoezi hayo kama tahadhari.
Pia wakati wa kuanza mazoezi hayo katika uwanja wa Krestovsky, Benjamin Pavard na N'Golo Kante walikuwa wakifanya mazoezi pembeni ya kikosi wakiwa wanakimbia taratibu kuzunguka uwanja chini ya usimamizi wa makocha wengine wa timu hiyo ya Ufaransa.

(Getty Images) Source: Getty
Nusu fainali za michuano hiyo ya Dunia inatarajia kuanza kuunguruma alfajiri hii kwa saa za hapa Australia pale Ufaransa itakapokabiliana na Ubelgiji na nusu fainali ingine kuchezwa keshokutwa alfajiri ambapo Uingereza itamenyana na Kroatia.
Michezo yote hii itaonyesha na runinga yako ya SBS moja kwa moja kutoka Urusi.