Timu ya wanaume ya mchezo wa 'squash' kutoka Sierra Leone na mkufunzi wa wanyanyua vyuma toka Rwanda, wamo miongoni mwa Waafrika wanamichezo walitoweka katika michuano ya Jumuiya za Madola mjini Gold Coast.
Hii inakuja ndani ya masaa machache yaliyopita baada ya Waziri wa mambo ya ndani Peter Dutton kuwaonya wanariadha watakaovunja sheria juu ya vibali vyao vya kusafiria kuwa watatafutwa na kukamatwa kisha kurudishwa nchi zao.
Wanamichezo Ernest Jombla na Yusif Mansaray kutoka Sierra Leone, hawakuonekana kwenye mchezo wao wa pamoja leo Alhamis asubuhi.
Hii ina maana, Jombla na Mansaray walishindwa kuhudhuria michezo yao mjini Gold Coast baada ya kutoonekana siku ya Jumanne kwa mchezo dhidi ya Peter Creed na Joel Makin kutoka Wales.
Licha ya wawili hao kutoonekana katika michezo yao, Maafisa wa Sierra Leone walisisitiza kuwa, wawili hao walikuwa bado kwenye kijiji hicho cha michezo ila walichanganyikiwa na mida ya michuano yao.
Naye afisa mwandamizi wa Rwanda, Eugene Nzabanterura amesema, mkufunzi wao Jean Paul Nsengiyuma hajaonekana tangu kumalizika kwa mchezo wake katika kiwanja cha Carrara Sports siku ya Jumanne.

Cameroon's Simplice Fotsala Source: AAP
Taarifa zingine zilitolewa kuhusiana na kutoonekana kwa wanamichezo wengine Waganda wawili , lakini maafisa wa timu yao walidai wanamichezo wao na viongozi wote wapo.
Taarifa hizi zinakuja siku moja baada ya wanamichezo wanane kati ya 42 wa Cameroon kutoweka, ikijumuishwa mabondia wawili ambao hakauonekana kwenye mapambano yao.
Wanariadha wengi wako kwenye viza zinazowaruhusu kukaa nchini hadi tarehe 15 mwezi wa Tano lakini Dutton alitilia mashaka kutokuonekana kwa wanamichezo hao kwenye michezo ya mashindano yao ikiwa hayo ndiyo yaliyowaleta.

Minkoumba Petit David of Cameroon competes during Men's 94kg final of Weightlifting on day four of the Gold Coast 2018 Commonwealth Games Source: Getty Images
Mkuu wa michezo ya Jumuiya za madola Peter Beattie alisema, ingawaje vibali vya kusafiria wanamichezo hao vinawaruhusu kutembea popote na kufurahia Australia, ila wanatakiwa kurudi nchi zao kama ilivyopangwa.
Share

