Morocco ili ingia katika mechi ya nusu fainali dhidi ya bingwa watetezi Ufaransa ikiwa imebeba matumaini yama milioni yamashabiki kutoka barani Afrika, uarabuni na hata waumini wa dini laki Islamu kote duniani.
Licha yakumiliki mpira kwa sehemu kubwa ya mechi hiyo, bahati ili tabasamu kwa upande wa wafaransa ambao walifanikiwa kufunga goli mbili zilizowapa ushindi.
Muda mfupi baada ya mechi hiyo kuisha, Morocco ilimiminiwa jumbe zapongezi kutoka sehemu zote za dunia, na hata kutoka kwa Rais wa Ufaransa aliye watembelea wachezaji ndani ya chumba chao chakubadilishia nguo kuwapongeza kwa juhudi zao.
Hongera Morocco kwa kuwakilisha Afrika vyema.