Scott Morrison na Bill Shorten wamekabiliana kwenye suala la wanaotafuta hifadhi, gharama za sera na magari ya umeme katika mjadala wa viongozi wa kwanza wa kampeni ya uchaguzi wa shirikisho leo Jumatatu usiku huu.
Hakukuwa na mshindi wa wazi wa mjadala ambao waliona viongozi wakijibu maswali juu ya uaminifu, kodi, hali ya hewa na ulinzi wa mpaka.
Bwana Morrison aliulizwa kama amesema uongo wakati alisema mapema mwaka huu kwamba kutakuwa na wingi wa wanaotafuta hifadhi.

Prime Minister Scott Morrison arrives for the first leaders debate of the campaign. Source: AAP
Lakini waziri mkuu hakuwa na uhakika kwa swali hilo.
"Hiyo ilikuwa ni ushauri wa katibu wa masuala ya mambo ya ndani, "Bwana Morrison aliwaambia watazamaji, kabla ya kuendelea kusema kuwa kufunguliwa kwa kituo cha kizuizini cha kisiwa cha Krismasi kimetenda kama kizuizi.
Kituo hiki kimepangwa kufungwa mwezi wa Julai bila kuwa na mwombaji hifadhi yeyote au mkimbizi kwenda kisiwani humo.
Bwana Shorten kwa upande wake pia alivutiwa juu ya rekodi ya chama chake cha Labor juu ya sera ya mpaka na alisema sasa amekubaliana na sera ya serikali juu ya kugeuza mashua kuzuia vifo katika bahari.

Opposition Leader Bill Shorten arrived for the debate with his wife Chloe Shorten. Source: AAP