Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Chama cha Waislamu chalaani shambulio baya la kigaidi lililofanywa na Wanamgambo wa Kiislamu nchini Burkina Faso

Shirikisho la chama chaKiislamu nchini Burkina Faso limelaani shambulio baya la Kigaidi lilofanywa na wanamgambo wa Kiislamu wenye msimamo mkali nchini humo.

Forensic workers in protective clothing and Burkina Faso soldiers examine the Splendid Hotel in Ouagadougou, Burkina Faso, Sunday, Jan. 17, 2016.
Forensic workers in protective clothing and Burkina Faso soldiers examine the Splendid Hotel in Ouagadougou, Burkina Faso, Sunday, Jan. 17, 2016. (AP Photo/Sunday Alamba) Source: AP

Shirikisho la chama chaKiislamu nchini Burkina Faso limelaani shambulio baya la Kigaidi lilofanywa na wanamgambo wa Kiislamu wenye msimamo mkali nchini humo.

Majeruhi katika tukio hilo, lilotokea katika hotel ya kisasa mjini Ouagadougou, amesema wanamgambo hao walikuwa wakiwalenga wazungu.

Vikosi vya Usalama vikiongozwa na jeshi la Ufaransa na Marekani, vilisaidia kuirudisha hotel katika himaya ya usalama baada ya masaa kadhaa ya operetaion hiyo ambapo wanamgambo wanne waliofanya mashambulizi hayo waliuawa papo hapo.

Wakati mateka 150 wakiachiliwa huru, takribani watu 23 kutoka mataifa 18 walifariki dunia katika shambulio hilo , huku mmoja wa waliojeruhiwa akisema wanajihadi hao walirudi mara kwa mara katika hoteli hiyo maarufu kwa watalii ili kuwapiga tena risasi majeruhi waliokuwa wamelala chini kwa kunyanyua meza na viti.

Sheikh Sidi Mohamed Saday kutoka shirikisho la Burkina Faso chama cha Kiislamu alisema, shambulio hilo linahitaji kukemewa.

Alisema, "Kama raia wa Burkina Faso, na vile vile Muislamu - tumehudhunishwa sana na mashanbulizi haya. Baadhi ya watu wameliteka jina la Kiislamu. Hatuutambui Uislamu katika matendo haya. Tunalaani ushenzi huu. Haiwezi kuelezewa na dini yoyote."


1 min read

Published

Updated

By Biwa Kwan, Frank Mtao

Source: SBS News



Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now