Bw Mudavadi alieleza vyombo vya habari kupitia tangazo hilo kuhusu hitilafu nyingi, zinazo husiana na matokeo ya uchaguzi yaliyo kuwa yaki tangazwa na IEBC kwa upande wa uchaguzi wa urais.



Taarifa ya chama cha muungano wa NASA kwa vyombo vya habari Source: NASA Kenya

Taarifa ya chama cha muungano wa NASA kwa vyombo vya habari Source: NASA Kenya

Taarifa ya chama cha muungano wa NASA kwa vyombo vya habari Source: NASA Kenya
Akizungumza kwa niaba ya muungano wa NASA, Bw Mudavadi amedai chama chake kime pokea matokea halisi ya uchaguzi wa urais kutoka mtu mmoja ndani ya tume la IEBC. Matokeo hayo yame baini kuwa kinara wa NASA Bw Raila Odinga ana kura nyingi zaidi ya mpinzani wake Bw Uhuru Kenyatta.
Bw Mudavadi, ameleza tume ya IEBC itangaze rasmi Bw Odinga kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais wa 2017. Kwa mujibu wa Bw Mudavadi, hesabu halisi za kura za urais ndani ya mitambo ya IEBC, zime mpa Bw Raila Odinga kura 8,056,885 ilhali Bw Uhuru Kenyatta ana kura 6,659, 493.
Hata hivyo, tume ya IEBC ime sisitza uhuru wayo na kwamba, ita tangaza matokeo rasmi itakapo kuwa tayari.