Mtu mmoja mwenye kisu, amewaua watoto tisa wa shule za msingi na kujeruhi wengine 10 wakati wakiwa wanarudi majumbani huko Kaskazini China siku ya ijumaa, maafisa walisema, ni tukio kubwa la kutisha kutokea katika miaka ya hivi karibuni.
Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa na watoto waliojeruhiwa walikuwa wakipatiwa matibabu, alisema afisa wa usalama wa umma eneo la Mizhi kupitia mtandao wa kijamii.
Wasichana saba na vijana wa kiume wawili waliua katika tukio hilo, kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua, wakiwanukuu polisi wa eneo hilo. Umri wa watoto haukutajwa, lakini umri wa wanafunzi wa shule ya msingi inakadiriwa kuwa ni kati ya 12 na 15 nchini China.
Kwa mujibu wa maafisa usalama wa umma walisema, mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Zhao kutoka kijiji cha Zhaojiashan kitongoji cha Mizhi alikamatwa.
Walisema, mtuhumiwa alikiri kuwa, alikuwa akidhihakiwa na kuzomewa wakati akiwa anasoma darasa la tatu akiwa mdogo, hivyo aliwachukia wana darasa wenzake na kuamua kutumia kisu chenye ncha kali kuwaua watu siku ya Ijumaa.
Share

