Maofisa hao, wanahusishwa na kuchukua hongo kutoka kwa raia wa Naijeria ili kuwapa vibali vya kuishi.
Gazeti la The Herald Sun limetoa taarifa kuwa, takribani raia 21 wa Naijeria, walipata viza za Australia za uanafunzi ambapo uchunguzi wa hali wa kina ulibaini, maofisa wala rushwa wanidara hiyo ndio walifanikisha zoezi hilo.
Gazeti hilo liliendelea kubainisha kuwa, Idara ya mambo ya ndani ilithibitisha kuwa, raia wawili wasio Waustralia, wanaofanya kazi Ubalozi wa Australia nchini Afrika Kusini wamefukuzwa kazi.
Maofisa hao wanatuhumiwa kuwapa visa watu wanaoshukiwa kuwa hatari Australia pasipo kupitia hatua muhimu za uangalizi wa maombi.
Viza hizo 21, zilipitishwa mnamo mwezi wa pili hadi wa nne mwaka jana, kwa mujibu wa hati ya rufaa ya mahakama.
Hati hiyo inasomeka kuwa, viza hizo zilitambulika kupitishwa kupitia rushwa kutoka kwa maofisa wa idara hiyo.
Share

