Mvua hizo kubwa zilizoanza kunyesha asubuhi ya Jumatano, zimeelezewa kuwa kama ’mojawapo ya tukio katika matukio ya miaka 100’ na hazijaisha bado.
Rob Taggart kutoka Idara ya Hali ya Hewa aliliambia shirika la habari la ABC kuwa, hii ni siku ya mvua kubwa kuliko siku zote za mwezi wa kumi na moja tangu 1984 na ni siku ya mvua kubwa tangu mwezi wa nne 2015.
Alifafanua kuwa, mvua hizo zitaendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya Sydney mchana wa Jumatano baada ya zile za asubuhi.
Askari wawili walijeruhiwa wakati wakisaidia kumuokoa mmoja wa madereva aliyekumbwa na mafuriko wakati mvua kubwa zikizusha mtafaruku katika jiji la Sydney.
Askari hao walikuwa wakisaidia gari iliyokwama katika barabara ya Pittwater kitongiji cha Ryde Kaskazini mnamo majira ya saa moja asubuhi wakati mti ulipowaangukia.
Inasemekana, askari huyo anahofiwa kuvunjika mguu na Afisa mwingine yuko kwenye uchunguzi wa kina kama kuna uwezekano wa kupoteza fahamu.
Madereva wameonywa kutokuendesha magari ikiwa mvua kubwa za zaidi ya makadirio ya mwezi zikinyesha katika maeneo ya Sydney kwa takribani masaa mawili tu.
Share

