Taarifa kutoka tume ya uchaguzi nchini Rwanda, zinasema kwamba Paul Kagame ameshinda uchaguzi mkuu wa uraisi kwa 98.63% ya kura. Mpinzani wake wa karibu Philippe Mpayimana alipata 0.73% ya kura naye Frank Habineza alipata 0.47 ya kura.

Matokeo ya kura ya urais Rwanda Source: NEC Rwanda
Rais Kagame na familia yake walijiunga na mamia yama elfu ya raia wa Rwanda, katika vituo vyaku piga kura, kuamua atakaye ongoza taifa hilo kwa miaka saba ijayo.
Wanyarwanda wanao ishi Australia, nao pia walishiriki katika uchaguzi huo.

Rais Kagame aweka kidole wino kabla ya kupiga kura Source: Paul Kagame
Rais Kagame amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba, na sasa atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba. Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2015, na kumpa Rais Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka 2034.
Wafuasi wake wanamsifu kwa kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo mamia yamaelfu ya watu waliuaawa.
Share

