Kufuatia michuano hiyo iliyojawa na msisimko, fainali iliyofanyika mjini Moscow katika uwanja wa Luzhniki Stadium ulithibitisha hayo pale vijana wa Ufaransa maarufu kama 'Les Bleus' walipoanza kuzifumania nyavu za wapinzani wao katika dakika ya 18 kwa goli la kujifunga mwenyewe mchezaji Mario Mandzukic ambaye alikuwa shujaa wa dakika za nyongeza kwenye mtanange wa ushindi wa timu yake ya Kroatia dhidi ya Uingereza.
Kwa upande wa vijana wa Ante Dalic, walianza kwa nguvu na kufanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa Ivan Perisic kabla ya mshambuliaji huyo wa Inter Milan kuambiwa ameunawa mpira kwenye eneo la penati baada ya mfumo wa waamuzi wa akiba wa VAR kutumika katika fainal hizo.
Griezmann alipachika bao lake la nne katika michuano hiyo akiwa umbali wa yadi 12 kabla ya Kroatia kuwashambulia tena wapinzani wao kwenye mwanzo wa kipindi cha pili.
Hitilafu ambayo haikutarajiwa kutoka kwa golikipa mahiri Hugo Lloris, ilimruhusu mshambuliaji Mandzukic kuandika jina lake kwenye ubao wa magoli, lakini haikumzuia Didier Deschamps kuweka historia kama mwanasoka wa tatu kushinda Kombe la Dunia akiwa kama mchezaji na Kocha. Deschamps alikuwa nahodha wa kikosi cha Les Bleus waliponyakua kombe hilo mwaka 1998.