Konstebo Mwandamizi mwenye umri wa miaka 38 alishatkiwa kwa kosa la kuua siku ya jumamosi asubuhi, ikiwa ni miezi 18 kupita tangu mwanaye wa kiume mwenye umri wa miezi miwili kukutwa na majeraha katika kitongoji cha Victoria Point mjini Brisbane mashariki.
Askari huyo alikuwa amesimamishwa kazi lakini akiendelea kulipwa mshahara wake kamili lakini hili litapiwa tena baada ya sasa kushtakiwa.
Naibu kamishana wa polisi Queensland, Steve Gollschewski aliwahutubia waandishi wa habari...
Alisema "Kulikuwa na majeraha kadhaa kwa mtoto. Makosa kama haya ya jinai, kufuatia na aliyeyatenda ni maafa na ya kutisha. Ninaweza kusema tu ya kwamba, tumezingatia kama tunavyozingatia katika ajali hii ili kuhakikisha kwamba mkosaji anafikishwa mbele ya sheria."
Askari huyo, alitarajiwa kufikishwa mahakama kuu ya Brisbane leo hii.

