Kiwango cha joto la siasa nchini Kenya kimeongezeka baada ya mrengo wa Azimio One Kenya Alliance kufanya tangazo ambalo limetikisa taifa hilo la Afrika Mashariki.
Katika hotuba yake, kinara wa mrengo huo Mhe Raila Odinga alisema lazima pawe usawa wa jinsia na kwa sababu hiyo, amemteua kiongozi wa chama cha NARC Kenya, Martha Karua kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu baadae mwaka huu.