Viongozi hao walikuwa na jukumu la kuchagua kati ya Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Madagascar Richard Randriamandrato, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti, Mahmoud Ali Youssouf.
Matarajio ya Raila Odinga kushinda wadhifa huo yalipokea pigo kupitia barua ya katibu mkuu wa SADC, iliyo tangaza kuwa nchi wanachama wa muungano huo watampigia kura mwanachama wao kutoka Madagascar, Richard Randriamandrato.
Tangazo hilo lili maanisha Bw na Raila na Bw Mahmoud, walikuwa wamepoteza kura walizo tarajia kutoka wanachama wa SADC.
Baada ya raundi kadhaa za kura, Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti, Mahmoud Ali Youssouf ili ibuka mshinidi wa uchaguzi huo na ata hudumu kwa miaka minne ijayo.