Alipo hotubia umati wa wanachama wa mrengo wa Azimio One Kenya, Bw Odinga aliweka wazi sababu zaku pinga tangazo la mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Kenya IEBC.
Akisimama bega kwa bega na mgombea wake mwenza Martha Karua, pamoja na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Bw Odinga alisisitiza kuwa mrengo wake wa Azimio, utatumia kila mbinu yaki katiba na sheria kupata suluhu kwa azma yao. Bw Odinga, aliwaomba wakenya pia wadumishe amani na utulivu, pamoja naku wahakikishia wafuasi wake kuwa, hata kubali mtu mmoja ajaribu kubadili maamuzi ya wakenya.