Makamu wa rais wa zamani Kalonzo Musyoka, ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha Wiper Democratic Movement, ameteuliwa kuwa mgombea mwenza wa bwana Odinga.
Image
Bwana Odinga sasa atakabiliana na Rais Uhuru Kenyatta, atakayetumia chama cha Jubilee kuwania muhula wa pili.
"Hii ni heshima kubwa sana ambayo ndugu zangu wamenifanyia, kwa kuniweka nipeperushe bendera ya NASA. Tumekuwa na vikao ambavyo vimechukua siku nyingi. Kila kitu tumeandika.”
Bwana Odinga alisema wakati akihutubu baada ya kutangazwa kuwa mgombea wa NASA.
Kikosi hicho cha NASA kilitangazwa jana Alhamisi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara ulioandaliwa katika bustani ya Uhuru mjini Nairobi.

Viongozi wa chama cha mseto cha NASA Source: Raila A Odinga
Wanachama wengine wakuu watatu wa muungano wa NASA Musalia Mudavadi, Moses Wetangula na Isaac Ruto, nao wamepewa nyadhifa za juu katika muungano huo, ambazo watatekeleza ikiwa watashinda urais kwenye uchaguzi wa Agosti.
Ikiwa watashinda, waziri mkuu mratibu wa shughuli za serikali atakuwa kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi.

Bango la chama cha Mh Musalia Mudavadi Source: Musalia Mudavadi
Naibu waziri mkuu mratibu wa uchumi atakuwa kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula.
Image
Kiongozi wa Chama cha Mashinani (CCM) Isaac Ruto atakuwa naibu waziri mkuu atakayesimamia utawala na huduma za jamii.
Image
Share

