Nyota wa mashindano hayo hadi sasa ambaye anaendeleza pale alipoishia baada ya kupiga magoli matatu dhidi ya Uhispania katika mechi ya ufunguzi iliyokwenda sare ya 3-3 kwa Kundi B, aliwapelekea vijana wa Fernando Santos kupata bao la kuongoza kwa goli lililomfanya afikie magoli 85 ya kimataifa - goli moja zaidi ya mkongwe Ferenc Puskas katika orodha ya wafungaji bora.
Kocha wa Morocco Renard, aliingia mchezoni huku akiwa ameona wachezaji wake wakikosa pointi baada ya kutawala sehemu kubwa ya mchezo wa mwanzo dhidi ya Iran, waliweza kufanya vizuri pia kwenye mchezo huu, wakiwa wamefanikiwa kuwafanya Ureno kukaba kwa muda mwingi huku wakipunguza makali ya mshambuliaji hatari Ronald.

Cristiano Ronaldo of Portugal disputes as Dirar from Morocco during the match at the Lujniki stage during the 2018 World Cup championship. Source: Ale Cabral / AGIF (via AP)
Morocco watakuwa na nafasi ya kurudisha heshima yao kwa kupata matokeo mazuri ya mchezo wao wa mwisho Kundi B dhidi ya Uhispania na baadaye kurudi makwao wakiwa wamehudhunishwa na kutokuonyesha mazuri katika mechi zake mbili nchini Urusi, wakati Wareno walipiga hatua kubwa kuelekea kwenye hatua ya timu za mwisho 16.
Wakati huo huo,
Misri imeondolewa kwenye michuano hiyo ya Kombe la dunia baada ya mechi mbili tu
Wamisri waliwasili Urusi wakiwa na mchezaji mahiri Mohamed Salah na wakiwa na matumaini makubwa.
Timu hiyo inacheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990, ilikuwa na matumaini ina uwezo wa kupata matokeo mazuri, hata Salah akiwa bado anaugulia kuumia bega. Lakini baada ya mechi mbili, Wamisri walishaondolewa kwenye kinyanga’anyiro.
"Daima huwa nasema, nyuma ya mchezaji kuna timu," Kocha wa Misri Hector Cuper alisema siku ya Jumanne baada ya kichapo cha bao 3-1 toka kwa mwenyeji Urusi. "Nina faraja, tulikuwa na timu, lakini hatukuwa na maamuzi ya kutosha."
Salah aliumia mwezi uliopita katika fainali za michuano ya mabingwa Ulaya. Alivaa jezi kwenye mechi ya ufunguzi lakini aliwekwa akiba wakati Misri wakiwashikilia Uruguay kutokufunga hadi dakika ya 89.

Egypt star Mohamed Salah Source: Getty Images
Hatimaye, hata hivyo, Uruguay ikafunga na kushinda mchezo huo.
Salah alianza kucheza mechi ya pili dhidi ya Urusi na hata kufanikiwa kufunga kutokana na penati, lakini taifa mwenyeji walithibitisha kuwa wababe.
Kupoteza mechi hizo mbili na ukijumuisha ushindi wa Urusi pamoja na Uruguay dhidi ya Saudi Arabia, ilihitimisha timu hiyo ya Afrika Kaskazini kuondolewa licha ya kubakiza mchezo mmoja wa mwisho Kundi A utakaopigwa siku ya Jumatatu.
Matumaini makubwa na muasha washa woote, ulikuwa juu ya mchezaji mwenye umri wa miaka 26 Salah, ambaye alifunga magoli 44 katika mechi 51 kupitia timu yake ya Liverpool na alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa ligi hiyo ya Uingereza.