Joto la siasa nchini Kenya limekuwa likiongezea kila siku, na mrengo wa Kenya Kwanza uliteka fikra na hisia za taifa hilo kwa masaa kadhaa, mgombea wao Naibu Rais William S Ruto aliposoma hotuba ndefu na hatimae akamtangaza mgombea wake mwenza Rigathe Gachagua.

Prof Kindiki katika kampeni ya UDA Source: Kithure Kindiki
Bw Gachagua alikuwa akiwania wadhifa huo dhidi ya mwanasheria wa Bw Ruto, Prof Kithure Kindiki. Imeripotiwa kuwa sikumoja kabla, wawili hao walishiriki katika mazungumzo magumu yakujaribu kutatua swala la atakaye mgombea mwenza wa Bw Ruto bila mafanikio.