Huduma za SBS Radio zabadilishwa kuzingatia mahitaji ya mabadiliko nchini Australia

Baada ya tathmini ya huduma ya Radio ya SBS, lugha saba mpya ziki jumuisha, Rohingya, Tibetan na Telugu, zita pewa vipindi vyao binafsi katika radio ya SBS, wakati baadhi ya vipindi vingine vina sitishwa. Lengo la mabadiliko hayo, niku tosheleza mahitaji ya jamii ya Australia ya leo.

Tathmini ya huduma za SBS Radio

Tathmini ya huduma za SBS Radio Source: SBS

SBS imetangaza mabadiliko kwa huduma yake ya redio, yenye lengo laku timiza mahitaji ya jami toka tamaduni tofauti nchini Australia pamoja naku wakilisha ongezeko la jamii mbali mbali nchini.

Matokeo ya data ya sensa mpya, imeonesha idadi ya watu wapatao kati ya milioni 4.87 na milioni 5 ya wakazi nchini huzungumza lugha ambayo ni tofauti na kiingereza nyumbani.

Tathmini ya huduma za Redio SBS zime zingatia matokeo ya sensa mpya pamoja na jinsi wasikilizaji wanavyo pokea taarifa.

Idadi ya watu wanao sikiza matangazo ya lugha, viwango vya uelewa wa Kiingereza, muda jamii husika ilipo wasili nchini, umri na rasilimali nyumbani nazo pia zili zingatiwa.

Na visa vya ubaguzi wa jamii yoyote nchini Australia, pia ulizingatiwa.
Thathmini ya huduma hizo ita jumuisha lugha saba mpya zikiwa, Telugu, Karen, Tibetan, Hakha Chin, Rohingya, Mongolian na Kirundi.
Makala yote ya lugha hizi mpya yatapatikana kupitia mitambo yakidijitali kupitia makala yaliyo rekodiwa kwa on-demand, na unaweza yasikiza kupitia tovuti ya SBS na kwenye app ya SBS Redio.

Mkurugenzi wa redio katika shirika la SBS, Mandi Wicks amesema ni muhimu kwa SBS Radio kuwakilisha Australia ya leo.
Tuna furaha tuta ongeza lugha saba mpya katika huduma zetu za radio kama sehemu ya tathmini tuliyo fanya. Moja ya lugha hizo mpya ina itwa Telagu, ambayo inazungumzwa na idadi ya watu wapatao milioni 74 India. Kwa hiyo tuna furaha kuiongeza katika huduma zetu za redio. Ni jamii change, ambayo 74% ya watu wana umri wa miaka kati ya 20-54. Kwa hiyo tuna tazamia kuwa hudumia nakuwasaida wanapo anza maisha yao mapya katika nchi mpya.
SBS ilipokea zaidi ya maoni 600 kutoka jamii zinazo zungumza lugha takriban 85 wakati, wa mchakato wa ushauriano wa umma kutoka Novemba hadi Disemba mwaka jana.

Mchakato huo wa ushauriano uliwapa watu binafsi pamoja na mashirika fursa, yaku changia maoni yao, kwa vigezo vya uteuzi vilivyo pendekezwa.

Hatimae maoni hayo yali zingatiwa vigezo vilipo kamilishwa.

Moja ya kigezo kilicho jumuishwa, kili tizama kama lugha inayo zungumzwa na kundi fulani, ina zungumzwa na watu wengi, na idadi ya watu hao ni angalau takriban elfu 25.

Vigezo vya lugha zenye mahitaji makubwa, vili zingatia jamii zenye idadi ya watu elfu 1, pamoja naku zingatia ujuzi wao wa kiingeeza, wakati walipo wasili nchini, umri wa wana jamii pamoja na rasilimali nyumbani mwao.

SBS ilizingatia pia mahitaji ya jamii zingine na kama mahitaji hayo yalikuwa hayaja shughulikiwa ipasavyo na vigezo vingine.

Baadhi ya mambo yaliyo zingatiwa yalijumuisha, ubaguzi nchini Australia kwa misingi ya rangi, kabila au mtu anakotoka.

Mahitaji ya haraka nayo yalizingatiwa, iwapo kume kuwa ongezeko katika idadi ya watu wanao zungumza lugha fulani kupitia mradi wa uhamiaji wa wakimbizi.

Lugha 12 zita sitishwa kupitia vigezo vya mwisho.
Lugha zitakazo futwa katika huduma ya SBS Radio zina jumuisha; Kannada, Tongan, Norwegian, Cook Island Maori, Fijian, Swedish na makala ya kiingereza kwa jamii zawa Afrika.
Badala ya hizo lugha, SBS ita hudumia lugha saba mpya, Rohingya na Kirundi ziki jumuishwa.

Vipindi katika lugha zaki Lithuanian, Malay, Latvian, Danish na Maori zime kuwa katika mapumziko kwa muda wa miezi 12 hadi 18 iliyo pita nazo pia zita sitishwa.

Huduma ya taarifa kwa kiingereza kutoka SBS World News Radio, kuanzia sasa ita tolewa kupitia mitambo yaki dijitali pamoja na makala yaliyo rekodiwa. Makala yakila siku kwenye redio nayo yata sitishwa pia.

Mandi Wicks amesema ni changamoto yakila wakati kuhakikisha SBS inatoa makala yanayo stahili na yanayo wafikia watu wengi.
Nadhani moja ya changamoto kuhusu mabadiliko ya haraka nchini australia, katika miaka mitano iliyo pita ni baadhi ya jamii si kubwa kama zilivyo kuwa ukizilinganisha na jamii zingine. Zime pitwa pia kwa upande wa idadi ya watu. Tulipo tazama vigezo vya tathmini hii, kwa bahati mbaya kulikuwa baadhi ya lugha ambazo haziku timiza vigezo mwaka huu wa 2017. Kwa hiyo kwa bahati mbaya, baadhi ya lugha hizo zita sitishwa kufikia mwisho wa mwaka huu.
Joe Caputo ndiye mwenyekiti wa FECCA, hilo ni shirika linalo wakilisha jamii kutoka tamaduni tofauti. Amesema ni muhimu kwa SBS kuendelea kuzingatia mbinu zaku hudumia jamii vizuri.
Nadhani ni muhimu kwa SBS kuhakikisha inaendelea kuwa muhimu kwa jamii za tamaduni tofauti nchini Australia ambazo zina endelea kubadilika kwa upande wa ongezeko la watu wapya, kwa upande wa jamii ambazo zina ishi na zime kuwa ziki ishi nchini kwa muda mrefu. Kwa hiyo nadhani tathmini hizi ni sehemu muhimu kwa jinsi SBS inafanya kazi, na inapo endelea kuhakikisha ina tekeleza mahitaji ya jamii za tamaduni tofauti zinapo endelea kupitia mabadiliko.
Mabadiliko yame fanywa pia, kwa masaa ya matangazo ya baadhi ya lugha.

Masaa ya vipindi katika lugha zaki Turuki naki Kroeshia, yata pungua kutoka masaa matano hadi masaa mane kila wiki wakati makala katika lugha yaki Jerumani yata pungua kutoka masaa saba hadi masaa tano kila wiki.

Vipindi katika lugha zaki Hungarian, Bosnian na Albanian nazo zita pungua naku fanya matangazo mara moja kila wiki.

Mabadiliko pia yame fanywa kwa masaa ya matangazo ya baadhi ya lugha kama, Dari, Dinka, Khmer, Maltese, Nepali, Pashto na Tigrinya.

Mandi Wicks ameongezea kwamba, lengo la SBS niku endelea kufanya tathmini ya huduma zake kila miaka mitano kwaku zingatia data za sensa mpya.
Kimsingi tuko hapa kuwa siliana na jamii na wahamiaji kuhusu maisha hapa Australia, na kuhusu jamii wanamo ishi. Hali hii ina endelea kubadilika. Na kuna jamii mpya zinazo endelea kuwasili kila wakati ambazo zina hitaji huduma zetu kuelewa mifumo yetu, kuelewa maadili ya Australia pamoja naku anza maisha upya katika nchi mpya.
SBS Radio itaendelea kuwa shirika lenye matangazo katika lugha tofauti mbali mbali, iki peperusha makala katika lugha 68.

Mageuzi hayo yata anza kutumika kuanzia tarehe 20 Novemba.


Share

4 min read

Published

By Hannah Sinclair

Presented by SBS Swahili

Source: SBS




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service