Waziri Mkuu Scott Morrison na Kiongozi kambi ya upinzani wanajiandaa kukabiliana na mjadala muhimu kama kura za maoni za hivi karibuni zinaonyesha Serikali ya Umoja huo inapata unafuu.
Kura za maoni hizo zilizochapishwa na gazeti The Australian siku ya Jumapili usiku, zimeonyesha serikali iko na asilimia moja tu nyuma ya Upinzani katika maoni ya chama kipi kipewe kipaumbele baada ya kuanza kwa nguvu kwa kipindi cha wiki tano za kampeni.
Bwana Morrison anaingia katika mjadala kwa kasi huku wengi wakibashiri kuboreshwa katika uchaguzi kutokana na utendaji wake wenye nguvu katika kampeni za uchaguzi.
Bwana Morrison ametilia mkazo shambulizi lake kwa Upinzani ambapo amekejeli mipango ya kodi ya chama cha Labor na kumshambulia Bill Shorten kwa kumuita "dubu mwenye hasira".
Lakini, kura za awali zinaonyesha serikali ya Umoja imeshuka asilimia moja hadi kufikia asilimia 38, wakati chama cha Labor kiko chini kwa asilimia 37