Imefahamika "ScoMo" - ambaye alikuwa Waziri wa Fedha tangu mwaka 2015 - ameshinda kwa kura 45 kwa 40 katika mkutano wa chama ambao ulikuwa ukilazimisha kuondoka kwa Waziri Mkuu wa sasa Malcom Turnbull.
Josh Frydenberg ameteuliwa kuwa Kiongozi msaidizi wa chama cha Liberal kwa maana ndiye Waziri Mkuu Msaidizi.
Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Peter Dutton, Waziri wa mambo ya nje Julie Bishop na Bwana Morrison walikuwa kwenye ushindani huo leo hii mchana kupitia chama chao cha Liberal.

Wagombea wa uongozi wa chama cha Liberal na wadhifa wa waziri mkuu wa Australia, Scott Morrison, Julie Bishop na Peter Dutton. Source: AAP
Kabla ya mkutano huo wa shinikizo, wahamiaji wengi walikuwa wamezizunguka ofisi za Bunge mjini Canberra huku wakipinga kuwemo kwenye kinyang'anyiro hicho cha Uwaziri Mkuu Bwana Peter Dutton.
Peter Dutton akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alionyesha kuwa mkali zaidi kwa Wahamiaji kuingia nchini na ndiye aliyehaidi swala la Uhamiaji nchi hii kuwa ndiyo kipaumbele chake kama atateuliwa kuwa Waziri Mkuu.

Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, na mgombea wa wadhifa wa waziri mkuu Peter Dutton, awasili bungeni kupiga kura yaku ahirisha vikao vya bunge. Source: AAP
Wengi wa waandamaji, walimfananisha Peter Dutton kama Donald Trump, wa Marekani kutokana na kauli zake za hapa na pale.
Share

