Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Utafutaji wa ndege iliyoanguka baharini waendelea

Utafutaji wa ndege ndogo iliyoanguka baharini Victoria na kuua watu wote wanne waliokuwemo, umeendelea kuanzia jana.

A Victorian Police boat is seen docked at Point Lonsdale following a plane crash at Barwon Heads in Victoria. AAP Image/Mal Fairclough)
Police boat with the 3 recovered bodies that are believed to have died after a plane crashed at Barwon Heads in Victoria. AAP Image/Mal Fairclough) Source: AAP

Licha ya kuongezeka muda huo wa kutafuta katika kina kirefu chini ya bahari eneo la Point Lonsdale, bado mabaki ya ndege hiyo kwa jina la Piper Cherokee iliyoanguka baharini siku ya ijumaa hayajapatikana.

Miili ya watu watatu ilipatikana masaa machache tu baada ya ajali hiyo lakini mwili wa mtu wa nne haujapatikana.

Polisi wamesema, huenda ikawa mwili huo umejifunga ndani ya mabaki ya ndege hiyo takribani mita 30 chini ya usawa wa bahari katika eneo la utafutaji la ukubwa wa mita 500.


1 min read

Published

Updated

By Frank Mtao

Source: SBS News



Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now