Waziri Mkuu Malcolm Turnbull amethibitisha taarifa hiyo akiwa pamoja na Seneta Gichuhi kupitia video iliyo chapishwa kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Katika video hiyo, Bw Turnbull ame mweleza Seneta Gichuhi ambaye ni mzawa wa Kenya kwamba:
"Lucy, hadithi ya maisho yako inatia moyo, ni hadithi yakujituma, kufanya kazi kwa bidii na uhuru. Na maadili yako niyaki Liberal."
Kwa upande wake, Seneta Gichuhi alimjibu waziri mkuu kwamba:
"Ndio, siku gundua hali hiyo hadi nilipo toa hotuba yangu ya kwanza. Nili fikiri, 'Wow - siwezi amini jinsi nilivyo mliberal kimsingii, na nadhani hali hiyo ina nisaidia kuwahudumia watu wa Kusini Australian." Image
Ujio wa Seneta Gichuhi ni taarifa nzuri kwa serikali ya mseto, hali ambayo ina piga jeki idadi ya kura ndani ya seneti hadi 30.
Hatua hiyo imerejeshea serikali ya mseto idadi ya viti ilivyo poteza katika nyumba ya juu bungeni, kabla Cory Bernardi ahame kutoka chama tawala.