Seneta huyo wa chama cha Liberal, Lucy Gichuhi huenda akafikia kikomo kwa kazi zake za kisiasa kufuatia taarifa kuwa atashushwa hadi nafasi ya nne katika uchaguzi ujao kwa upande wa chama chake eneo la Kusini mwa Austalia.
Waziri Mkuu Malcolm Turnbull amemuelezea Seneta Mkenya huyo kama mtu wa mfano mzuri baada ya kujitenga kutoka chama cha Family First na kujiunga na chama cha Liberal mnamo mwezi wa pili lakini uhamisho huo unaweza kumfanya kupoteza kiti chake bungeni.

File: Senator Lucy Gichuhi defected to the Liberal party Source: Twitter/Malcolm Turnbull
Kitengo cha haki cha chama hicho, hakikumkubali kijamii seneta huyo na kitaangalia uwezekano wa kumrudisha Mkuu wa mji wa Adelaide Alex Antic juu ya Seneta huyo kwa tiketi hiyo. Taarifa za shirika la habari la ABC zilifafanua hivyo siku ya Jumanne.
Waziri msaidizi wa masuala ya Maji na Kilimo, Anne Ruston anatarajiwa kuchukua nafasi ya kwanza wakati Seneta David Fawcett au Bwana Antic kati ya mmoja wapo kushika nafasi ya pili - huku wakimuacha Seneta Gichuhi kupambana kurudisha kiti chake akiwa kwenye nafasi isiyowezekana, nafasi ya nne.
Seneta mpya wa Kusini Australia, Lucy Gichuhi akiapishwa ndani ya Seneti ya taifa mjini Canberra, Australia Jumanne 9Mei2017 Source: Picha: AAP/Mick Tsikas
Share

