Bingwa mara sita, alihitaji saa moja na dakika 45 kumchakaza Muitaliano Camila Giorgi kwa alama 6-4 7-5 katika hali ya hewa ya joto kali siku ya kwanza ya michuano hiyo.
Kuumia kwa goti kumlizuia Williams kushiriki mashindano tangu yale ya wazi ya Marekani mnamo mwezi wa tisa, lakini Muamerika huyu alikuja bila kujeruhiwa kupata tiketi yake ya mzunguko wa pili utakaochezwa siku ya jumatano ambapo atakutana na kati ya Mlatvia, Jelena Ostapenko au Mtaiwani, Su-Wei Hsieh.
Williams aliliambia runinga ya Channel Seven kuwa, aliridhishwa kwa kupewa mtihani huo mzuri katika mchezo wake wa kwanza kwenye michuano hiyo maarufu kama 'Australian Open'.
Alisema, "Yeah, haikuwa rahisi. Bila shaka alicheza vizuri sana na anajua kuupiga vyema mpira. Na sijacheza mchezo wowote wa mashindano kwa muda mrefu sana, lakini nafikiri ilikuwa vizuri kwangu kuja hapa na kufanikiwa kuendelea mbele. Na haikuwa haraka, na hilo kwa kweli lilikuwa kwa manufaa yangu pia."

