Wapiga kura walijumuika katika vituo vyakupigia kura kote nchini, baadhi yao wakiwa wame fanya maamuzi tayari ya watakaye mchagua na wengine wakifanya maamuzi katika sekunde za mwisho kabisa.
Licha ya ahadi zote ambazo vyama vikubwa vilitoa katika kampeni za uchaguzi mkuu, mpiga kura alikuwa na maamuzi magumu yakufanya kuhusu hatma ya uongozi wa nchi. Na baada ya vituo vya kura kufungwa na hesabu kuanza kutangazwa, serikali ya mseto imejipata pabaya baada ya matokeo ya mapema kupendelea upinzani wa shirikisho.
Kufikia wakati wakuchapisha taarifa hizi, chama cha Labor kilikuwa kikiongoza kwa kura 71 kiki hitaji kushinda viti vitano ili kiweze unda serikali bila msaada wa vyama vingine. Wakati huo huo serikali ya mseto imeshinda maeneo bunge 49 na inamlima mrefu mbele yake iwapo itasalia mamlakani.
SBS Swahili ita endelea kukupa taarifa mpya kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu, punde tatakapo yapata.

Waziri Mkuu Scott Morrison, akiwa katika kampeni ya uchaguzi mkuu. Source: AAP

Kiongozi wa upinzani Anthony Albanese, kwenye uzinduzi wa kampeni ya chama cha Labor. Source: Getty

Baadhi ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa Australia Source: SBS Swahili