Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE starting June 12 2026

Mwongozo wa makazi: 5 muhimu kuhusu mradi wa AMEP

Mradi wa mafunzo yakiingera kwa wahamiaji ambao ni watuwazima (AMEP) ndio mradi mkubwa zaidi nchini Australia wa makazi, unao toa zaidi ya masaa 500 ya mafunzo ya kiingereza kwa wahamiaji wapya.

Settlement Guide: 5 facts on AMEP
Ramani na watu wanao ishi nchini Australia Source: Getty Images

1 Idadi kubwa ya watu wanao wasili nchini na viza yaku dumu au ya muda, hufuzu kujifunza kiingereza darasani bila malipa.

Mradi wa AMEP hutolewa bila malipo kwa kila mtu ambaye ana viza yakudumu na kwa baadhi ya watu ambao wana viza ya muda ambao hawana kiwango stadi cha kiingereza.

Australian visa
Source: SBS

2 Wamiliki wa viza zinazo fuzu wanastahili kujiandikisha kushiriki katika mradi wa AMEP, katika muda wa miezi sita baada yaku wasili nchini Australia.

Watu ambao wana umri wa chini ya miaka 18 wana muda mrefu wakujiandikisha na wanafunzi wote wanastahili kumaliza masomo ndani ya muda wa miaka mitano.

New arrivals

3 Cheti kutoka masomo hayo hukubalika kitaifa, kwa sababu kina toa ushahidi kuwa mmiliki ana ujuzi wakusoma nakuandika Kiingereza.

Kuna viwango vinne vya masomo, vikianzia masomo ya msingi hadi yakati.

Accredited courses

4 Kuna namna nyingi yaku fanya masomo hayo katika maeneo mengi.

Masomo yanaweza fanywa kila siku, siku chache ana kwa ana na walimu, au mtu anaweza somea kwa mbali au nyumbani, mtandaoni au mwalimu anaweza mtembelea mwanafunzi nyumbani. Idadi ya rmashirika ambayo yame sajiliwa kutoka huduma hiyo yanaweza patikana katika maeneo 250 nchini Australia.

Classroom

5 Wanafunzi wanaweza tumia huduma zaku lea watoto bila malipo iwapo wana watoto ambao hawaja anza shule.

Wanao toa huduma ya AMEP wana wajibu waku andaa huduma ya watoto kwa wateja wao ambao wana watoto ambao hawaja anza shule.

Childcare
Source: AAP

Maelezo kuhusu Mradi wa mafunzo ya Kiingereza kwa wahamiaji ambao ni watu wazima yana weza patikana katika lugha 26.

 

 


1 min read

Published

Updated

By Ildiko Dauda

Presented by Gode Migerano




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now