Watch FIFA World Cup 2026™ LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Mwongozo wa Makazi: Mambo 5 muhimu yakujua kabla yaku toa ripoti mtu anapo potea

Nchini Austrlaia mtu yeyote anaweza ripotiwa kwa polisi iwapo mahali alipo hapajulikani, na kuna wasi wasi mkubwa kuhusu usalama na ustawi wao. Polisi watakapo pokea ripoti hiyo, wata fanya uchunguzi nakujaribu kumpata mtu huyo ambaye amepotea. Kwa hiyo unapashwa fanyaje, iwapo mtu unaye mjua anapotea?

Bango la kituo cha polisi

Bango la kituo cha polisi Source: AAP

1. Si lazima usubiri masaa 24 kuwasilisha ripoti mtu anapo potea.

Iwapo unawasiwasi kuhusu usalama, ustawi wa mtu, na mahali alipo hapajulikani, unaweza toa ripoti maramoja kwa polisi, sehemu unako ishi kwaku toa ripoti ya mtu ambaye amepotea.

Missing person
Source: Yui Yui Hoi/Getty Images

2. Ripoti ya mtu ambaye amepotea, inaweza tolewa katika kituo cha polisi kilicho karibu yako.

Ripoti zinazo wasilishwa kupitia simu zinakubaliwa tu katika mkoa wa Kusini Australia. Wasiliana na kituo cha polisi unako ishi kujadili mahitaji yako kama hauwezi fika katika kituo cha polisi kuwasilisha ripoti yako.

Missing persons
Source: Australian government

3. Toa maelezo kamili unapo wasiliana na polisi.

Itakuwa msaada mkubwa kwa polisi ukiwapa maelezo yakutosha kumtambua mtu ambaye amepotea. Maelezo hayo nikama; majina, maelezo ya mawasiliano ya marafiki wake, aina ya mapato yao ya Centrelink, maelezo ya pasipoti, mahitaji ya matibabu na maswala mengine yanayo kupa wasiwasi kuhusu ustawi wao.

Missing person in water
Source: AAP

4. Unapo wasilisha ripoti ya mtu ambaye amepotea, huenda polisi wata chukua maelezo kamili mara moja.

Polisi wanaweza fanya uchunguzi nakuwasiliana nawe uwape maelezo ya ziada, iwapo mtu huyo hajapatikana katika muda mfupi.

Missing people poster
Source: Rattlenoun CC BY SA 4.0

5 Hifadhi rekodi ya ripoti unayo wasilisha.

Huenda ikakufaidi kuhifadhi taarifa ifuatayo- namba ya uchunguzi wa tukio, kituo cha polisi na jina na cheo cha afisa mhusika.

New South Wales Police badge
Source: AAP

Hati zenye maelezo zinapatikana katika lugha 14 tofauti. Kwa maelezo ya ziada tembelea Australia’s tovuti rasmi ya Australia ya watu ambao wame potea.

Unaweza piga simu kwa namba hii bila malipo: 1800 000 634.

Kama unahitaji mkalimani pigia simu shirika la wakalimani TIS kwa namba hii: 13 14 50.

Tovuti yaku sajili watu ambao wame potea nchini Australia hotoa maelezo bila malipo na lengo lake niku toa taarifa kuhusu watu ambao wame potea kutoka mikoa na kanda zote nchini Australia.

Maelezo yaziada yanaweza patikana hapa: Watu ambao wame potea: Mwongozo kwa familia na marafiki wa watu ambao wame potea.

 


1 min read

Published

Updated

By Gode Migerano, Ildiko Dauda

Presented by Gode Migerano




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now