Watch FIFA World Cup 2026™ LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Mwongozo wa makazi: Mfumo wa serikali

Chini ya mfumo wa shirikisho wa Australia, mamlaka yame gawanywa kati ya serikali ya kati na serikali za mikoa. Bunge la taifa linajumuisha Malkia ambaye huwakilishwa na Gavana Mkuu, Seneti na Nyumba yawa wakilishi. Serikali ya taifa ya Australia, hugawanywa katika vitengo vitatu: bunge, mamlaka na mahakama. Je vitengo hivi hutumikaje?

Parliament House in Canberra

Source: Getty Images

1. Nchini Australia, mamlaka hugawanywa kati ya serikali ya taifa, mkoa na majimbo.

Sheria za taifa zinazo tungwa na bunge, lazima zipitishwe ndani ya nyumba zote mbili za bunge zikiwa ni: Nyumba ya wawakilishi na katika Seneti. Sheria hizo lazima zitiwe saini na Gavana Mkuu.

Queen Elizabeth with Governor-General
Source: AAP

2. Mara nyingi Nyumba ya Wawakilishi bungeni huitwa, Nyumba ya Chini, ina jumuisha wabunge wapatao 150 kutoka nchi nzima.

Nyumba hiyo huamua chama kitakacho unda serikali, pia hupitisha sheria, hufuatilia utendakazi pamoja naku jadili maswala yenye umuhimu kwa taifa. Baada ya uchaguzi mkuu, serikali huundwa na chama ambacho kina wabunge wengi ndani ya nyumba ya chini bungeni. Kiongozi wa chama chenye idadi kubwa yawa wakilishi ndani ya nyumba ya chini, ndiye huwa Waziri Mkuu.

House of Representatives
Source: AAP

3. Seneti ama kama inavyo julikana mara nyingi, Nyumba ya Juu, ina jumuisha idai ya wanachama wapatao 76, kumi na mbili kutoka kila mkoa, na wawili kutoka majimbo mawili nchini. Jukumu kuu la Seneti niku chunguza miswada inayo tumwa kutoka Nyumba ya Chini ya bunge la taifa. Maseneta hu hudumu kwa mihula ya miaka 6, wakati nusu yama seneta huchaguliwa kila miaka mitatu ama katika uchaguzi mkuu.

Senate
Source: Getty Images

4. Serikali ya taifa la Australia hugawanywa katika vitengo vitatu: bunge, utawala na mahakama.

Bunge la Australia, lina jumuisha wawakilishi ambao wame chaguliwa kwa misingi ya demokrasia nchini kote. Wajibu wa bunge niku jadili nakupigia kura sheria mpya ambazo huwasilishwa chini ya mamlaka ya kitengo 51 cha Katiba.

Federal Parliament
Source: Getty Images

Mtendaji ni mkono wa utawala wa serikali. Wajibu wayo niku tunga naku tekeleza sheria zilizo imarishwa na bunge.

Front bench ministers
Source: AAP

Mahakama ni mkono wa sheria wa serikali, ni huru na tofauti na bunge na mamlaka. Jukumu lake niku hakikisha sheria za Australia zina fuatwa. Lazima pia ihakikishe mikono mingine ya serikali haikiuki mamlaka ya katiba.

Scales of justice
Source: Getty Images

5. Nchini Australia serikali ya taifa huchaguliwa kupitia kura, ambayo ni lazima kwa kila raia.

Uchaguzi wa taifa hufanywa kila miaka mitatu. Uchaguzi mkuu ujao utafanywa katika vituo zaidi ya 8000 nchini kote, tarehe 2 Julai kuanzia saa mbili asubui hadi saa 12 jioni. Raia wa Australia wote, wenye umri wa miaka 18 na zaidi wanapashwa jiandikisha nakupiga kura.

Australia votes
Source: Getty Images

Kwa maelezo ya ziada kuhusu kuhusu mfumo wa taifa wa Australia tembelea tovuti hii: Australian Government’s

Kwa maelezo ya jinsi yaku piga kura tembelea tovuti hii: Australian Electoral Commission’s

Tafsiri ya maelezo kuhusu jinsi yakupiga kura yanaweza patikana hapa: your language.


1 min read

Published

Updated

By Ildiko Dauda




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now