Mashabiki wa Shujaa (Kenya) wali wasili katika michuano ya Sydney7s wakiwa na matumaini yaku shuhudia nchi yao ikishinda moja ya kombe zilizo kuwa zikiwaniwa.

Mashabiki wa shujaa, katika michuano ya Sydney7s 2019 Source: SBS Swahili
Matarajio hayo yalisababishwa na jinsi Shujaa ilivyo cheza katika michuano ya Hamilton, New Zealand ambako Kenya ilishinda mechi tatu naku shindwa katika mechi mbili.
Hata hivyo matarajio hayo yali zimwa kwa haraka kufuatia matokeo kadhaa mabaya ambayo Shujaa ilipata, nakusababisha kenya kumaliza michuano ya Sydney7s bila kushinda hata mechi moja.

Mashabiki wa shujaa, waonesha hisia zao katika michuano ya Sydney7s 2019 baada ya Kenya kuondolewa katika michuano hiyo. Source: SBS Swahili
Mashabiki wengi ambao SBS Swahili ilizungumza nao, wali sikitishwa kwa jinsi Kenya ilivyo cheza katika michuano ya Sydney7s, hata hivyo wengi wao walikuwa na matarajio chanya kwa timu hiyo iliyo jawa vijana wengi chipukizi.

Jacob Ojee Nahodha wa Shujaa Kenya, ndani ya uwanja wa michuano ya Sydney7s 2019 Source: SBS Swahili
Tulipo zungumza na nahodha wa Shujaa Bw Jacob Ojee, naye pia ali elezea masikitiko yake pamoja na machezaji wenzake katika michuano hiyo.
Bw Ojee aliwashukuru mashabiki kwaku endelea kuwa na imani na timu, pamoja naku washabikia na ali ahidi kuwa timu yake, ita fanyia kazi mafunzo waliyo pata katika michuano ya Sevens inayo salia.

Mashabiki wa shujaa, katika michuano ya Sydney7s 2019 Source: SBS Swahili
Matokeo mabaya ya Shujaa katika michuano ya Sydney7s hayaku vunja mioyo yawa Kenya kabisa, maana wali endelea kushabikia timu zilizo salia katika michuano hiyo.
New Zealand ili onesha umahiri wake uwanjani, ambako timu zake za wanaume na wanawake walinyakua ushindi wa michuano ya Sydney7s 2019.
Share

