Ushindi huo ulipatikana kwa jasho baada ya mshambuliaji wao maarufu Sadio Mane, kushindwa kufunga penati katika dakika ya sita ya fainali hiyo dhidi ya bingwa mara saba wa Afrika Misri.
Hata hivyo Mane hakufa moyo na yeye na wachezaji wenza walionesha viwango vyao pamoja na vipaji, kwaku tawala fainali hiyo kwa muda mrefu hatakama hawakufanikiwa kufunga goli lolote katika muda wa masaa mawili ya mechi hiyo.
Upande wa pili wa fainali hiyo alikuwa Mo Salah, mchezaji ambaye kwa sasa anazingatiwa kuwa mchezaji bora wa soka duniani ambaye pia hucheza pamoja na Mane katika kikosi cha Liverpool, Uingereza. Hata hivyo, urafiki uliwekwa kando kila mmoja wao akitetea nchi yake katika mechi hiyo.