Waandamanaji Sudan wagomea mazungumzo huku vifo vikifikia 100

Idadi ya waliofariki kutokana na vurugu ya wanajeshi dhidi ya waandamanaji wa demokrasia nchini Sudan imeripotiwa kufikia 100

A tire burns at a roadblock in the center of Khartoum, Sudan.

A tire burns at a roadblock in the center of Khartoum, Sudan. Source: EPA

Viongozi wa maandamano wa Sudan siku ya Jumatano walikataa ombi la baraza la kijeshi la mazungumzo huku wakidai haki kwa vurugu ambazo madaktari wamesema umeacha watu 101 kufariki dunia.

 
Vikosi vya usalama viliamini kuwa ni pamoja na wajumbe wa zamani wa Janjaweed, wanasiasa wa serikali ambao waliishtua dunia juu ya dhuluma huko Darfur, waliofanya ukatili katika maandamano siku ya Jumatatu.

 
Kamati Kuu ya Madaktari wa Sudan karibu na harakati za maandamano walisema Jumatano kuwa, takribani watu 101 wameuawa katika vurugu hizo, ikiwa ni pamoja na miili 40 iliyopatikana kutoka mto Nile.
A protester wearing a Sudanese flag in front of burning tires and debris on road 60, near Khartoum's army headquarters
A protester wearing a Sudanese flag in front of burning tires and debris on road 60, near Khartoum's army headquarters Source: AP
Sudan inaongozwa na halmashauri ya kijeshi baada ya kumuondoa madarakani rais wa zamani Omar al-Bashir mwezi Aprili baada ya waandamanaji wakidai aondoke uongozini kabla ya kukubaliana na kipindi cha miaka mitatu ya mpito kwa utawala wa kiraia.


Share

Published

Updated

By Frank Mtao

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service