Hali ya hewa ya mvua na wasiofika kazini kutokana na kuumwa, vimelalamikiwa kusababisha ucheleweshaji wa muda mrefu wa treni mjini Sydney leo hii.
Wasafiri siku ya Jumatatu, wamejikuta wakiamka na kukuta kusitishwa kwa huduma kadhaa katika mtandao wa reli za Sydney, wakati mamlaka ya usafiri wakilaumu "suala la uendeshaji".
"Huduma zimebadilika asubuhi hii zinaweza kukuathiri, kutokana na hali ya hewa ya mvua na idadi kubwa ya watumishi kuwa wagonjwa, "Sydney Trains waliandika kwenye mtandao wao wa tweeter Jumatatu asubuhi ya leo.
Ucheleweshaji unaathiri huduma kwenye Reli ya Kaskazini T1, Magharibi ya kati T2 na Leppington, T3 Bankstown, T5 Cumberland na treni ya kusini ya Airport T8, na hivyo mabasi kuongezwa kusaidia wasafiri.
"Treni zinaendelea kufanya kazi katika njia hizo lakini unaweza kukutana na ucheleweshaji kwa hivyo jipe muda wa ziada wa kusafiri, "msemaji wa Kituo cha Usimamizi wa Usafiri Dave Wright aliiambia redio ya ABC.
Share

