Jumanne, Australia iliripoti vifo 55 vya UVIKO-19, 20 vikiwa New South Wales (NSW), 16 Victoria na 15 Queensland.
Kesi za kila siku pamoja na wanao lazwa hospitalini wameongezeka katika majimbo na wilaya za Australia.
Tazama maendeleo mapya ya UVIKO-19 kwa kesi mpya, wanao lazwa hospitalini na wanao fariki nchini Australia hapa.
Meli ya abiria wenye maambukizi ya UVIKO-19 pamoja na wafanyakazi, kwa sasa ina elekea katika bandari ya Eden ambayo iko katika pwani ya kusini ya NSW kutoka Brisbane, Queensland. Meli hiyo inatarajiwa kuwasili Sydney Jumatano.
Idara ya afya ya NSW imesema idadi ndogo ya abiria wana maambukizi ya UVIKO-19 ndani ya meli ya Coral Princess. Kuna uwezekano abiria hao wali ambukizwa kabla yakuabiri meli hiyo, kisha baadae wakapatwa na virusi hivyo.
Idara hiyo imeongezea kuwa maambukizi mengi yako miongoni mwa wafanyakazi wa meli hiyo. Mamlaka wamesema abiria wote watakao tua jimboni wata ombwa, warejeshe vipimo vya hasi vya RAT kwanza. wafanyakazi wa meli hiyo hawata ondoka ndani yake.
Majimbo ya NSW na Victoria yamekubali ushauri kutoka kamati kuu ya ulinzi wa afya ya Australia, kwa kupunguza muda wa maambukizi kutoka wiki 12 hadi siku 28. Jimbo la Magharibi Australia na wilaya ya Australian Capital Territory zilikuwa za kwanza kukubali ushauri huo jana Jumatatu.
Wakaaji wanao patwa na virusi vya UVIKO-19 baada ya siku 28m za maambukizi yao ya nyuma, sasa watahesabiwa kama kesi mpya katika majimbo hayo.
Afisa Mkuu wa Afya wa NSW Dr Kerry Chant, amesema virusi vya BA.4 na BA.5, ambavyo ni aina mpya ya kirusi cha Omicron, vinaweza epuka kinga kutoka maambukizi ya nyuma na chanjo ndani ya wiki kadhaa baada ya maambukizi ya nyuma.
Victoria iliripoti ongezeko ya 53% ya idadi ya watu ambao wame lazwa hospitalini kwa UVIKO-19, katika wiki mbili zilizo pita. Waziri wa Afya Mary-Anne Thomas amesema aina mpya ya virusi zinatarajiwa kuendelea kukuza maambukizi mapya, na wanao lazwa hospitalini.
Serikali ya jimbo hilo imetangaza raundi nyingine ya mradi wa ruzuku ya uingizaji hewa kwa biashra ndogo, kusaidia biashara ziwekeze kwa vifaa ambavyo vitasaidia kuhakikisha wafanyakazi na wateja wako salama ndani yamajengo.
Waziri Thomas amesema hakuna mageuzi kwa sheria zilizopo za uvaaji wa barakoa jimboni humo. Hata hivyo, amewahasisha waajiri wazingatie mipangilio yakufanyia kazi nyumbani kwa wafanyakazi wao. Amewahamasisha wakaaji pia wavae barakoa wakiwa ndani yamajengo.
Kerryn Coleman ni Afisa Mkuu wa Afya wa ACT, amesema idadi ya kesi za kila siku inatarajiwa kufikia kilele mwisho wa Julai au mwanzo wa Agosti. Amesema ACT inaweza shuhudia ongezeko la hadi kesi 3,000 kila siku.
Bi Coleman amesema hawana mpango wakurejesha amri yakuvaa barakoa.
Afisa Mkuu wa Afya wa Australia, Prof Paul Kelly, alieleza runinga ya ABC kuwa, baadhi yamajimbo yanaweza ahirisha upasuaji wakuchagua, wakati kuna kuwa ongezeko ya maambukizi ya UVIKO-19 na kesi za mafua.
Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya