Raisi wa Tanzania, John Magufuli siku ya Ijumaa, ameamuru kukamatwa kwa uongozi wa kivuko kilichozama maji katika ziwa Victoria, wakati idadi ya watu waliopoteza maisha ni zaidi ya 140 hadi sasa na waokoaji wanaendelea leo hii na utafutaji wa miili mingine iliyozama maji.
MV Nyerere huenda ilikuwa imebeba zaidi ya abiria 200 -- ikiwa ni idadi mara mbili ya uwezzo wa kivuko hicho -- wakati ikizama karibu na ufuko katika kisiwa cha Ukara siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.
Mashuhuda wa ajali hiyo waliongea na AFP walisema, kivuko hicho kilizama wakati abiria wakikimbilia upande mmoja ili kutoka kwa haraka ndani ya kivuko hicho wakati kikiwa kimekaribia kutia nanga.
Katika hotuba iliyorushwa na TBC ambayo ni Televisheni ya umma, Magufuli alisema "Inaonyesha wazi kuwa, kivuko hiki kilijaa kupita kiasi," akaongeza kuwa "uzembe umetughalimu maisha ya watu wengi.. watoto, akina mama, wanafunzi, Wazee".
"Ninaamuru kukamatwa kwa wote waliohusika na usimamizi wa kivuko hicho. Ukamatwaji huo umeshaanza," aliongeza.
Mh Raisi alitangaza siku nne za maombolezo kitaifa huku akitaja idadi ya watu waliopoteza maisha kufikia 131, ikiwa ni idadi zaidi ya ili ya awali ya watu 126 lakini leo hii wakati tunachapisha habari hii, shirika la habari la TBC lilitangza idadi hiyo kuongezeka na kufikia 140 na hadi kugikia jioni ya leo inatarajiwa idadi kuongezeka zaidi.
Shughuli za utafutaji miili zaidi umeendelea leo kuanzia alfajiri majira ya Tanzania na tayari Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Kassim Majaliwa amekwisha wasili eneo la tukio kuungana na waombolezji na vikosi vya uokoaji wa janga hilo kubwa kutokea.
Itakumbuka kuwa, mwaka 1996 pia janga kama hilo lilitokea katika ziwa hilo na kupoteza mamia ya maisha ya watu.
Share

