Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli hapo jana kwa masikitiko makubwa alitangaza kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa kilichotokea usiku wa kuamkia jana taraehe 24 Julai 2020.
Mhe. Rais Magufuli alisema, Mhe Banjamin Mkapa alifariki dunia hosptalini jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kuwa watulivu na wastahimilivu baada ya kupokea taarifa za kuondokoewa na mpendwa wao Mhe. Benjamini William Mkapa.
Mhe. Magufuli alisema, Watanzania walipkee hilo, wamepata msiba mkubwa na waendelee kumuombea Mzee wao Mstaafu Banjamin Mkapa ambaye ametangulia mbele za haki.
Kufuatia msiba huo mkubwa huo, Rais Magufuli alitangaza siku 7 za maombolezo ya Kitaifa kuanzia Ijumaa tarehe 24 Julai, 2020.
Mwili wa Marehemu Benjamin William Mkapa unatarajiwa kuzikwa Jumatano ijayo kijijini Mpaso wilayani Masasi mkoani Mtwara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, shughuli za kuaga zitafanyika kwa siku tatu kuanzia Jumapili na zitafanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.