Katika hotuba yake fupi, Makamu wa Rais alisema kwamba:
"Tarehe 17 Machi 2021 majira ya saa kumi na mbili jioni, tume mpoteza kiongozi wetu shupavu, Rais wa Muungano wa Jamuhuri ya Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli."
Aki elezea kilicho sababisha kifo cha Rais, Mhe Hassan alisema:
"Alifariki kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam akipatiwa matibabu. Mhe Rais Magufuli alilazwa tarehe 6 Machi 2021, katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, kwa tatizo la moyo la mfumo wa umeme ambalo alikuwa nalo kwa zaidi ya miaka 10." Image
Mhe Hassan anaye tarajiwa kurithi wadhifa wa mwendazake, ameongezea kuwa mipango ya mazishi inafanywa na Tanzania itakuwa katika kipindi cha maombolezo kwa siku 14 na mbendera zitapepea nusu mlingoti.
Mhe Dkt Rais John Pombe Joseph Magufuli, ni miongoni mwa viongozi kadhaa katika serikali ya Tanzania walioga dunia katika siku na wiki chache zilizopita, baadhi wakiripotiwa kufa kwa ungonjwa wa Coronavirus. Mhe Dkt Rais Magufuli ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 61.
SBS Swahili itakupa taarifa zaidi kuhusu tukio hili, punde tutakapo zipokea.