Tanzania inataka kuongeza idadi ya utalii kwa kuweka gari za waya kwenye Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kabisa wa Afrika na iko katika mazungumzo kuhusu mradi huo na kampuni ya Kichina na ya Ulaya.
Takribani watalii 50,000 hupanda mlima Kilimanjaro kila mwaka.
Gari za waya zitaongeza idadi ya watalii kwa asilimia 50 kwani itasaidia kufanya kuwa rahisi kuufikia mlima kwa wale wasioweza kupanda, Constantine Kanyasu, naibu waziri wa utalii alisema.
Nchi inafanya upembuzi kujua njia zinazowezekana kwa wakati huu, Kanyasu aliiambia Reuters.

A cable car has been proposed for Mount Kilimanjaro. Source: pexel
“Bado tunafanya utafiti wa ufanisi ili kuona kama mradi huu unafanya kazi,” Alisema.
“Kuna makampuni mawili kutoka China na nyingine kutoka nchi ya Magharibi ambazo zimeonyesha kuvutiwa.”
“Hii siyo kwa mara ya kwanza duniani, magari ya umeme yapo Sweden, Italy, Himalaya."
Kanyasu alisema, serikali ilikuwa inaangalia mipango ya biashara, nafasi za wawekezaji na faida.
Urefu wa njia haujahitimishwa, na chaguzi mbalimbali zinazingatiwa kulingana na mambo ya gharama na uhandisi, alisema waziri huyo.
Tathmini ya athari za mazingira pia zitafanyiwa kazi, alisema
Wasaidizi wa kubeba mizigo (Wapagazi) na vikundi vya waongozaji kupanda milima ambao huwatembeza watalii juu ya mlima wanapinga mradi kwa sababu wanaogopa magari ya waya yatapunguza idadi ya wapagazi hao.
Loishiye Mollel, kiongozi wa shirika la wapagazi Tanzania alisema, wageni kwa kawaida hutumia wiki moja kupanda mlima huo.
“Mgeni mmoja kutoka marekani anaweza kuwa na watu 15, ambapo 13 kati yao ni wapagazi, wapishi na waongozaji. Ajira zote hizi zitaathiriwa na magari ya waya,” Alisema.
“Mtazamo wetu ni kwamba, mlima unapaswa kuachwa kama ulivyo.”
Kuna takribani wasaidizi wa kubeba mizigo (wapagazi) 20,000 wanaofanya kazi kati ya Mlima Kilimanjaro na Meru, ambao ni mlima wa jirani, alisema.

Gondola transportation system carrying guests to the top of the Oakland Hills. Source: (Smith Collection/Gado/Getty Images)
Mapato ya Tanzania kutokana na utalii yaliongezeka kwa asilimia 7.13 mwaka jana, imesaidiwa na ongezeko la kufika kwa wageni wa kigeni. Mapato ya utalii yalileta $ 2.43 bilioni kwa mwaka, kutoka $ 2.19 bilioni mwaka 2017.
Utalii ni chanzo kikubwa cha fedha nchini Tanzania, inayojulikana kwa fukwe zake, safari za wanyamapori na Mlima Kilimanjaro, ambao una vilele vitatu vya volkano na uko karibu mita 5,000 kutoka chini.
Wazo la gari za waya halimvutii kila mtu, na watumiaji wengi wa Twitter wameonyesha hasira zao.
"Kwa hiyo, kuibukia Kili kwa gari za waya, wakati wa kutosha kwa cappuccino, kuacha duka la zawadi & selfies kadhaa. Rejea hoteli wakati wa chakula cha mchana. Kuna mtu yeyote mwingine anajisikia huzuni na mitazamo hii?" mtumiaji mmoja aliandika.
Mwingine alikuwa mkali zaidi: "Hapana, hapana na hapana. Ni wazo la kijinga."
"Nimekuwa na bahati ya kuupanda mlima huo wa kushangaza mara mbili, hadi sasa. Kupitia uzuri wake wa asili na gari za waya ni uhalifu," mtumiaji mwingine wa Twitter alisikika.