Watu kumi waliuawa na wengine takribani ya 10 kujeruhiwa wakati mwanafunzi akiwa na bunduki kufyatua risasi kwenye shule yake ya sekondari mjini Texas siku ya Ijumaa, Polisi walisema, ni tukio kubwa la mauaji shuleni nchini Marekani.
Kijana huyo mwenye siraha, ambaye alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji, alitambulika kwa jina la Dimitrios Pagourtzis, mwenye umri wa miaka 17 na mwanafunzi katika shule hiyo ya sekondari ya Santa Fe iliyopo mji wa Santa Fe, Texas.
Gavana Greg Abbott alisema, watu 10 waliuawa na wengine 10 kujeruhiwa kwa kile alichokiita "moja la shambulio la ajabu zaidi halijawahi kutokea katika historia za shule mjini Texas."

A handout photo made available by the Galveston County Sheriff Office shows a booking photo of Dimitrios Pagourtzis, 17, in Galveston Source: AAP
"Hakuna kitakachomuandaa mzazi kwa kumpoteza mtoto," Abbott aliwaambia waandishi wa habari huko Santa Fe, iliyopo maili 30 (50 kilomita) kusini mashariki mwa Houston.
Abbott alisema, mtuhumiwa huyo wa mauaji, alitumia bunduki ya baba yake iliyokuwa inamilikiwa kihalali.
Nyaraka za Houston zinasema Pagourtzis, zaidi ya bunduki aliyokuwa nayo, alikuwa pia na mabomu ya kutengeneza wakati akilivamia darasa mwanzoni mwa siku ya shule.
Gavana alisema kuwa, upekuzi ulifanywa kwenye makazi mawili na "vifaa mbali mbali vya milipuko" vilipatikana ikijumuisha "kifaa aina ya CO2" na aina ya Molotov cocktail.

Two women pray outside the family reunification site following a shooting at Santa Fe High School on Friday, May 18, 2018, in Santa Fe, Texas. Source: AAP
Alisema, jarida alilokuwa nalo mtuhumiwa linaonyesha kupendekeza, "akajisalimisha."
Abbott pia alisema, kulikuwa hakuna onyo lolote kwa mtuhumiwa huyo kabla ya tukio ingawaje aliwahi kuweka fulana kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook iliyokuwa na maandishi "Alizaliwa kuua".
Maafisa wa Polisi walikuwa wakiwahoji watu wawili ikijumuisha mmoja amnbaye "huenda akawa kwa kiasi fulani ameshiriki kwenye uhalifu huo," Aliongeza Abbott.
Hospitali eneo hilo ilisema, majeruhi wawili walikuwa kwenye hali mbaya sana, na mmoja wa aliyejuruhiwa ni Afisa wa Polisi.
Share

