Kocha wa Bayern Hansi Flick amekiri kuwa kiungo huyo hatokuwepo leo kwenye mchezo utakaopigwa Signal Iduna Park baada ya kulazimishwa kukosa mazoezi ya Jumatatu.
"Thiago hakufanya mazoezi," Flick alisema.
"Kwa bahati mbaya, ameondolewa kwenye mchezo huu. Siri ya mwisho juu ya kikosi kamili, ningependa kubaki nayo mwenyewe."
Thiago amekwisha cheza mara 23 katika ligi hiyo kwenye msimu huu lakini alikaa nje kwenye mchezo wa Jumamosi iliyopita kutokana na maumivu ya nyonga, ambapo Bayern iliichakaza Eintracht Frankfurt kwa mabao 5-2.