Donald Trump na Kim Jong-un wamepeana salamu nzuri na kupeana mikono wakati wakati wakijiandaa kuanza kwa mkutano utakaoshughulikia masuala ya muda mrefu ya nyuklia na kumaliza chuki iliyokuwa ikiwarudisha kwenye vita baridi.
Wawili hao, walishikana mikono chini ya ukuta wa Hotel hapo Singapore, kabla ya kukaa kwa kikao cha nusu siku kitakacholeta malengo makubwa kwa kanda hizo na dunia kwa ujumla.

Australian leaders hope there will be progress made at the summit between North Korea and the US. (AAP) Source: AAP
Huu ni mkutano wa kwanza kabisa kuwahi kufanyika kati ya vinara wakubwa wa masuala ya nyuklia na ulikuwa haufikiri kutokea miezi michache iliyopita wakati hofu ilipotanda ya kutokea kwa vita vilivyosababishwa na majaribio ya nyuklia na mabishano kati ya pande mbili.
Wawili hao walishikana mikono kwa sekunde kadhaa, huku Trump akionekana kumsogelea Kiongozi wa Korea Kaskazini na kumgusa bega lake la upande wa kuli.
Share

