Turnbull ataka umoja, baada ya Dutton kujiuzulu kutoka baraza lamawaziri

Waziri Mkuu Malcolm Turnbull, ametoa wito wa umoja ndani ya chama tawala, baada yakumshinda Peter Dutton kwa kura 13, katika kura ya kiongozi wa chama mapema hii leo.

Waziri Mkuu Malcolm Turnbull na waziri wazamani wa maswala ya nyumbani Peter Dutton

Waziri Mkuu Malcolm Turnbull na waziri wazamani wa maswala ya nyumbani Peter Dutton walipo zungumza na vyombo vya habari Source: AAP

Bw Turnbull ali ibuka mshindi katika kura ya ghafla ya uongozi ndani ya chama cha Liberal, ambako matokeo ya kura hiyo dhidi ya mgombea mwenza Dutton yalikuwa 48-35 kwa upande wa Bw Turnbull

Bw Dutton kwa sasa amejiuzulu kutoka wadhifa wake wa waziri wa maswala ya nyumbani, na atahudumu kama mbunge wa kawaida, kama ilivyo desturi ya ushikamano katika baraza la mawaziri. Hakuna mbunge mwingine aliye gombea nafasi ya kiongozi wa chama isipokuwa Bw Dutton. Naye Julie Bishop alichaguliwa kuendelea kuhudumu kama naibu kiongozi wa chama cha Liberal bila upinzani.

Kwa sasa waziri mkuu Malcolm Turnbull, ametoa wito kwa umoja na ameongezea kuwa hana chuki wala uhasama dhidi ya Bw Dutton.

"Hatuwezi ruhusu, kama nilivyo sema ndani ya mkutano wa chama leo, maswala yetu ya ndani kudhoufisha kazi yetu," Bw Turnbull ali eleza waandishi wa habari mchana wa Jumanne." Ina unda athari, athari halisi, kuwa Bill Shorten atakuwa waziri mkuu."

Bw Turnbull amethibitisha kuwa, "alimwalika" Bw Dutton asalie ndani ya baraza la mawaziri katika wadhifa wake kama waziri wa maswala ya nyumbani ila, Bw Dutton alikataa mwaliko huo.



Mweka hazina Scott Morrison ata hudumu kama kaimu waziri wa idara ya uhamiaji, polisi wa shirikisho pamoja na mashirika makuu ya ujasusi ya Australia.

Wakati huo huo upinzani ulifanya mkutano wa chama jumanne ila, hawaja toa maoni yao kuhusu matokeo ya kura ya uongozi katika chama tawala cha Liberal.

“Sijui jinsi Bw Turnbull anaweza jifanya ana ongoza taifa, ilhali kila mbunge ana mamlaka sawa yake," Bw Shorten alisema.

Shirika la habari la SBS, lime pokea taarifa kuwa, Bill Shorten aliwaeleza washirika wake kuwa wapiga kura wana uliza "nini kina endelea?"

 


Share

Published

Updated

By James Elton-Pym
Presented by Gode Migerano
Source: SBS News

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Turnbull ataka umoja, baada ya Dutton kujiuzulu kutoka baraza lamawaziri | SBS Swahili