Ndege ya abiria ililipuka moto siku ya Jumapili hivyo ikafanya kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Moscow wenye pilika nyingi, na kuua watu angalau 41 kulingana na taarifa za maofiosa.
"Ndani ya ndege kulikuwa na watu 78 ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa ndege hiyo," Kamati ya Upelelezi ilisema katika taarifa, mapema ilitangaza kuwa angalau wawili wa waliofariki walikuwa watoto.
"Kwa mujibu wa taarifa za sasa ambazo wachunguzi wanazo, watu 37 walinusurika"
Video ya kushangaza iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha ndege hiyo ya Kirusi ya Aeroflot, ikiwaka moto na moshi mweusi ukifuka kutoka kwenye sehemu kuu ya ndege hiyo, ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sheremetyevo.
Abiria walionekana kuruka kupitia milango ya dharura na miteremko ya maboya mbele ya ndege kukimbia kutoka ndege iliyokuwa ikiwaka moto huku moshi mkubwa mweusi ukifuka kuelekea angani.