Matukio matatu ya Ebola yamethibitishwa nchini Uganda - uthibitisho wa kuenea kwa mara ya kwanza kwa gonjwa hilo hatari kulizuka nje ya miapaka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kijana wa umri wa miaka mitano alifariki dunia usiku wa Jumanne, bibi yake alifariki mara moja baadaye, na kaka yake mwenye umri wa miaka mitatu ni muathirika wa tatu. Familia hiyo hivi karibuni ilivuka mpaka kutoka DRC.
Familia ya kijana huyo mdogo ilijipeleka yenyewe kwenye kliniki ya eneo hilo baada ya kuanza kuona dalili.
Matukio ya Uganda yalionyesha kuwa janga liliingia awamu ya "kutisha" na inawezekana kuenea zaidi na kuua watu wengi zaidi, mtaalamu mmoja wa magonjwa ya kuambukiza aliiambia Reuters.
Janga la sasa la Ebola lilianza mwezi Agosti mwaka jana katika eneo la mashariki mwa Kongo na tayari limeambukiza angalau watu 2062, na kuua 1390 kati yao.
Hadi sasa Save The Children wanasema, wizara ya afya ya Uganda imefanya kazi nzuri ya kuzuia virusi kufikia nchi hiyo, "Katika mpaka rasmi kuna vituo vya uchunguzi wa Ebola ambavyo vimekuwa na ufanisi sana. Wizara ya afya nchini Uganda wamekuwa mstari wa mbele katika jitihada za kuzuia Ebola kuvuka, kwa mafanikio makubwa.