Katika siku ya furaha na kupeana mikono ikiwa ni mkutano wao wa kwanza kwa viongozi hao baada ya kipindi kirefu, wamehaidi kufanya kazi kushughulikia masuala ya kinyukilia katika ukanda huo.
Wawili hao walitangaza hivyo siku ya Ijumaa kuwa mwaka huu, watafanya kazi na Marekani pamoja na China ili kutangaza tamko rasmi la kumaliza vita yao ya miaka ya 1950 na kutafuta makubaliano kuanzisha amani ya "kudumu" na "imara".
Tamko hilo litajumuisha ahadi za kuondoa silaha za maangamizi, kuacha vitendo vya ki uadui, kubadilisha mipaka yao kuwa ya eneo la amani na kutafuta mazungumzo na nchi zingine ikiwemo Marekani.
Hatahivyo shughuli zote za taifa lote la Korea Kusini zilisimama kwa muda ambapo viongozi hao wawili walisalimiana kwa mikono katikati ya mpaka wa mataifa hayo mawili.

Kim Jong-un's message that he wrote in the Peace House visitor's book. Source: AAP
Na baadaye watu walishangaa baada ya bwana Kim kumualika kiongozi wa Korea Kusini kuvuka kwa muda mfupi katika mstari wa mpaka wa mataifa hayo mawili kuingia Korea Kaskazini, kabla ya wawili hao kurudi tena Korea Kusini muda wote huo wakiwa wameshikana mikono.
Kuvuka kwa mpaka huo kwa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, kunamfanya awe kiongozi wa kwanza kukanyaga Korea Kusini tangu vita ya Korea ya miaka ya 1950-53
Naye Raisi wa Korea Kusini Moon Jae-in, amekubali kuutembelea Mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang mwaka huu.
Viongozi hao wawili walikutana na gwaride ambalo likikuwa limevalia nguo za kitamaduni upande wa taifa la Korea Kusini.

North Korean leader Kim Jong Un and South Korean President Moon Jae-in's historic handshake. Source: AAP
Wawili hao baadaye walielekea katika jumba la amani huko Panmunjom, eneo la kijeshi katika mpaka huo ili kuanza mazungumzo.
Historia mpya imeanza sasa katika mwanzo wa amani, ulisema ujumbe ulioandikwa na bwana Kim alioandika katika kitabu cha wageni ndani ya jumba hilo la amani.
Mkutano huo wa Korea unaonekana kuwa maandalizi ya mkutano kati ya Kim Jong Un na rais wa Marekani Donald Trump, mapema mwezi Juni, hatua isiokuwa ya kawaida kwani hakuna Rais wa Marekani ambaye aliwahi kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini.
Share

