Tume huru dhidi ya ufisadi ilitangaza leo asubuhi kuwa itafanya vikao vya umma, kuchunguza iwapo Bi Berejiklian alikiuka imani ya umma katika mahusiano yake na mbunge wa zamani Daryl Macguire.
Bi Berejiklian alikuwa katika mahusiano binafsi na mbunge wa zamani wa chama cha Liberal wa Wagga Wagga, ambaye alipatwa kuwa alitumia ofisi yake ya umma pamoja na rasilmali za bunge kujinufaisha kifedha.