Beki huyo, alipiga kichwa mpira wa kona iliyopigwa na Antoine Griezmann katika dakika ya 51 hivyo kufanya kuwepo mtanange wa mataifa ya Ulaya ambapo kikosi hicho maarufu kama Les Bleus kitaelekea mjini Moscow kwa mpambano kati ya Kroatia au Uingereza.
Walinda mlango Hugo Lloris na Thibaut Courtois wote walifanikiwa kuokoa michomo mingi katika kuhakikisha mchezo huo mkali ubaki bila kufungana.
Hata hivyo, Umtiti akaibuka mapema kwenye kipindi cha pili, kwa kufunga goli lake la tatu la michezo ya Kimataifa.
Ubelgiji walijitahidi kwa nguvu zote kusawazisha lakini akajikuta Roberto Martinez akiangalia kikosi chake kikiadhibiwa kipigo chao cha kwanza tangu michezo 25 hivi, hivyo kuondoa matumaini yao ya kushinda kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia yao kwa vijana wanaofahamika kama kizazi cha dhahabu kushindwa kufurukuta.

(Reuters) Source: Reuters
Kikosi ambacho kilipoteza ubingwa wa Ulaya mwaka 2016 kwenye ardhi ya nyumbani Ufaransa, watakuwa na lengo la kufanya vizuri mwaka huu nchini Urusi na hivyo kurudisha heshima iliyowekwa na kikosi cha mwaka 1998 ambacho kilimjumuisha Didier Deschamps, ambaye huenda akafuata nyayo za Mario Zagallo na Franz Beckenbauer kwa kushinda kombe la dunia kama mchezaji na pia kocha.